Saa chache baada ya Mahakama ya London Uingereza kubainisha ufisadi wa zaidi ya shilingi trilioni moja, Ikulu imeibua majina ya watu waliohusika na ufisadi huo na kuanza msako.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi  Ombeni Sefue aiwaambia waandishi wa habari jana kuwa Tanzania ilipaswa kurejesha asilimia 1.4 ya mkopo wake kwa Benki ya Standard ya Uingereza lakini ilipofika Tanzania, Benki ya Stanbic ikaeleza kuwa Tanzania inapaswa kulipa asilimia 2.4.

Alisema ongezeko hilo la asilimia moja ni sawa na shilingi za Tanzania bilioni 15 zililipwa kinyume cha sheria kwa kampuni ya kitanzania ya EGMA inayomililikiwa na Harry Kitilya, ambaye wakati huo alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Harry Kitilya

Harry Kitilya

Wamiliki wengine wa kampuni hiyo ni Gasper Njuu na aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Umma Tanzania na Dk. Fratern Mboya ambaye ameshatangulia mbele ya haki. 

Balozi Sefue alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kilitolewa kwenye akaunti ya kampuni hiyo muda mfupi baadaye.

Alisema kuwa Rais John Magufuli ameagiza wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Kwa mujibu wa Balozi Sefue, Benki ya Standard itailipa Tanzania kiasi hicho cha shilingi bilioni bilioni 15 kilicholipwa kama kosa kwa kuwa nakubaliano ya awali hayakutakiwa kumhusisha mtu wa kati (kampuni ya EGMA).

Kafulila Aanza Vizuri Kesi Yake Ya Kupinga Matokeo
TACAIDS: Mastaa Wa Bongo Wako Hatarini Kupata Virusi Vya Ukimwi