Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile amefariki Dunia leo.

Dkt. Likwelile alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Idara ya Uchumi na Ndaki ya Sayansi ya Jamii Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Dkt. Likwelile ni mume wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM, Vicky Kamata na alifunga ndoa na Vicky Kamata, Machi 19, 2016.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Likwelile amefariki dunia akiwa nyumbani kwake, Mbweni jijini Dar es Salaam.

RC Geita akerwa na ufujaji fedha za miradi, aagiza uchunguzi
Wananchi Kagera kufungiwa maji bure majumbani