Rushaynah, aliyekuwa mke wa Haji Manara ameeleza kuhusu uhusiano wake na msanii Harmonize, baada ya kusambaa kipande cha video kinachomuonesha akiwa nyumbani kwa mwanamuziki huyo, siku chache baada ya kuachana na mumewe.

Akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitangazwa kuwa balozi wa bidhaa ya urembo jijini Dar es Salaam, mrembo huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa alimtembelea Harmonize kama rafiki yake na sio vinginevyo.

Aidha, akizungumzia madai kuhusu sababu za kuvunjika kwa ndoa yake na Manara, tukio ambalo lilipata nafasi kubwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na umaarufu wa Manara ambaye aliwahi kuwa msemaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Simba na baadaye mhamasishaji wa Timu ya Yanga, alisema ni mambo ambayo yalimshinda na hakuwa tayari kuyaweka wazi.

Alipoulizwa kama alikubali kuolewa na Manara kwa sababu ya fedha na kwamba ndiyo sababu ya kuachana naye, alijibu, “kwani Manara ana fedha? Ana fedha za kawaida tu.”

Rushaynah aliwashauri wanawake wasiogope kuanza upya pale wanapoona uhusiano wa kimapenzi au ndoa imekuwa chanzo cha maumivu yasiyovumilika.

Ndege ya Precision yapata hitilafu, yasitisha safari
Tanzania yapunguza maambukizi mapya VVU