Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetoa hukumu ya kesi iliyomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, William Mhando na mkewe, Eva Mhando.

Mhando alikuwa akishtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi pamoja na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Kwa mujibu wa mashtaka hayo, Mhando alitumia cheo chake kuipatia zabuni za shirika hilo kampuni ya Santa Clara Supplies inayomilikiwa na yeye mwenyewe, mkewe pamoja na mtoto wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Mhando alifanya maamuzi ya kuipa zabuni kampuni hiyo ili hali anajuwa kuwa alikuwa na maslahi, kinyume cha Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilifikia uamuzi wa kumuachia huru Mhando na mkewe.

Hakimu Mkazi Hellen Riwa, akisoma hukumu hiyo kwa niaba ya Hakimu mwenye kesi hiyo, Kwei Lusema alisema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha juu ya matumizi mabaya ya ofisi kwakuwa Mhando alikuwa hahudhurii vikao vya maamuzi vya Bodi ya Tanesco.

Hivyo, Mahakama hiyo ilieleza kuwa hakukuwa na ushahidi unaoonesha kama alikuwa na ushahidi wa moja kwa moja kwa Bodi hiyo kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara, ambayo kimsingi yeye na familia yake ni wamiliki.

Ripoti: Watanzania wengi hawataki kazi, hutumia muda mwingi kulala, starehe
Mwakyembe: Bora watanzania Tufe…