Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia leo Julai 22, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha, ndugu wa familia wamethibitisha

Mdogo wa Anna Mghwira na marafiki zake wa karibu wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho leo.

“Ni kweli Mghwira amefariki mchana huu, alikuwa amezidiwa akawa amepelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU),” amesema mdogo wake.

Zaidi ya wiki moja iliyopita alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua ambapo baadaye hali yake kuwa mbaya alihamishiwa hospitali ya Mount Meru.

Itakumbukwa aliondoka madarakani baada ya kustaafu Mei 2021 pia, aliwahi kugombea kiti cha Urais kupitia ACT-Wazalendo mwaka 2015.

Agizo la Waziri kwa wamiliki wa kumbi za starehe
Jeshi la Polisi Mwanza limethibitisha kumshikilia Mbowe