Mwanasheria maarufu wa Chicago ambaye aliwahi kumchomoa R Kelly kwenye kesi ya kurekodi video ya ngono na msichana mdogo mwaka 2008, Ed Genson  amemgeuka na kueleza alichodai ni ukweli kuhusu sakata hilo.

Mwanasheria huyo mwenye umri wa miaka 77 ambaye sasa anasumbuliwa na saratani akiwa amepewa siku 90 za kuweza kuishi kwa mujibu wa madaktari wake, amesema kuwa R Kelly alikuwa na hatia kwenye makosa hayo lakini alitumia mbinu za kumtetea na kufanikiwa.

Ed Genson ameiambia The Sun kwenye mahojiano maalum, “R Kelly alikuwa na hatia kama kuzimu. Sidhani kama ameshafanya jambo la ajabu sasa kwa miaka.

“Ngoja nikupe siri, ilibidi nimpeleke kwa daktari kufanyiwa tiba ya kuondoa nguvu ya mihemko ya mapenzi (libido-killing shots), ndio sababu hawakumkuta na hatia au kumkamata,” aliongeza.

Akizungumzia uamuzi wa R Kelly kufanya mahojiano na CBS hivi karibuni kuhusu tuhuma zake wakati kesi ikiwa imeshafikishwa mahakamani, Genson alionesha kushangazwa na uamuzi huo kwani ni kama kuingilia utaratibu wa mahakama.

“Sijui ni kwanini alifanya hivi, sielewi labda mwanasheria wake ni mjinga. Anaweza kuwa [mjinga],” alisema.

R Kelly anakabiliwa na mashtaka ya kuwanyanyasa kingono wanawake wanne, watatu kati yao wakiwa wasichana wanaodaiwa kuwa waliokuwa chini ya umri wa miaka 18.

Mfalme huyo wa RnB amekana vikali tuhuma hizo dhidi yake akidai ni njama za kutaka kumdidimiza. Alimwaga machozi na kusimama mara kadhaa kwa hisia akijitetea kwenye mahojiano hayo.

Juzi, wanawake wawili ambao ni kati ya wasichana ambao wazazi wao walionekana kwenye makala ya ‘Surviving R Kelly’ walijitokeza na kuwapinga vikali wazazi wao hao wakidai wanataka kujipatia fedha tu.

Ndege ya Ethiopia yapata ajali
Video: Lowassa msiniulize kwanini nimerudi, atoa agizo kwa wapiga kura wake

Comments

comments