Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma inamshikilia aliyekua mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Dodoma, Robert Daniel Mwinje kwa tuhuma mbalimbali ikiwepo ya kughushi nyaraka.

Akizungumza na waandishi wa Habari hii leo Mkuu wa TAKUKURU Dodoma, Sosthenes Kibwengo amesema Mwinje anatuhumiwa kwa makosa matatu kula njama, kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo.

Amesema Mwinje,hakutenda makosa hayo pekeyake bali alishirikiana na muhudumu wa Ofisi ya CCM Wilaya, Nyembo Malemda ambapo wametenda makosa hayo kati ya tarehe 18 na 20 Oktoba 2019.

“Walighushi barua ya Uteuzi wa waomba uongozi ndani ya Chama na huku wakijifanya imetolewa na Uongozi wa CCM Wilaya”, alisema Kibwengo na kusisitiza kuwa ni kinyume na sheria ya Kanuni za adhabu Sura ya 16 Marejeo ya Mwaka 2018.

Malawi: Uchaguzi wa marudio kufanyika Julai 2
GSM wasitisha huduma Young Africans

Comments

comments