Aziz Juma Mohammed, aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar, amekutwa akiwa amefariki nje ya nyumba yake iliyoko Kijichi.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohammed Hassan Haji (pichani) amesema kuwa kifo cha Aziz kina utata na sio cha kawaida, hivyo jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.

Kamishna Haji amesema kuwa kwa sasa hawatatoa taarifa kwa kina hadi watakapokamilisha upelelezi.

“Naomba mtosheke na hapo kwa sasa, najua mnataka kujua kuhusu tukio hili na muda ukifika mtaelezwa kilichotokea,” Kamishna Haji amewaambia waandishi wa habari.

Aidha, Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi kutoka Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Unguja, Dkt. Msafiri Marijani amethibitisha kuwa wameupokea mwili wa Azizi na kuufanyia uchunguzi.

Dkt. Marijani ameeleza kuwa wamebaini kifo cha askari huyo wa jeshi la polisi sio cha kawaida lakini taarifa zaidi zitatolewa na vyombo husika.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 10, 2019
Bashe ampongeza Bashungwa, 'Nakutakia kila la kheri'

Comments

comments