Sadiki Andrew, Mkazi wa Muheza aliyekuwa akisakwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchinja amejisalimisha Polisi akikiri kutekeleza mauaji hayo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Walyamba amesema kuwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa anatafutwa tangu wiki iliyopita kwa tuhuma hizo, alijisalimisha katika kituo kikuu cha polisi wilaya ya Muheza.

Kamanda Walyamba alieleza kuwa mtuhumiwa huyo alisema kuwa aliamua kujisalimisha kwa kuwa anaishi na virusi vya ukimwi na hutumia dawa za ARV zinazopunguza makali ya virusi hivyo, hivyo aliona ni bora kujisalimisha ili aweze kupata dawa hizo hata kama yuko jela.

”Baada ya kuona kwamba hawezi tena kwenda kuchukua dawa hizo kwa sababu anasakwa kwa tuhuma za mauaji, aliamua kujisalimisha polisi ili awe huru kupata dawa hizo hata kama yuko jela,” Kamanda Walyamba alisema.

Mtuhumiwa huyo aliliambia jeshi hilo kuwa alichukua uamuzi wa kumuua mkewe kutokana na hasira baada ya kumfumania akiwa na mwanaume nyumbani kwao.

Taarifa za awali za polisi zilieleza kuwa mtuhumiwa huyo alimvizia mkewe akiwa amelala kitandani ndipo alipochukua kisu na kumkata shingoni na kusababisha kifo chake.

Mamadou Sakho Akaribia Mlango Wa Kutokea Anfield
Thomas Tuchel: Sikumpanga Aubameyang Kwa Sababu Binafsi