Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limemuondoa kwenye orodha (Rolls) ya wauguzi na wakunga Tanzania baada ya kumkuta na hatia Muuguzi, Valentine  Kinyanga, wa kituo cha afya Mazwi ambaye alilalamikiwa kwa kosa la kumpiga vibao mama aliyefika kujifungua kituoni hapo January 5, mwaka huu.

Akisoma hukumu hiyo mbele ya Wakili wa Serikali, Fortunatus Mwandu, Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Abner Mathube alisema kuwa Baraza limemtia hatiani mlalalamikiwa chini ya kifungu 26(a)(c) ya sheria ya uuguzi na ukunga kwa kosa la kwanza na la pili.

Mwandu aliongeza kuwa kutokana na hayo Baraza limempa adhabu ya kumuondoa kwenye orodha (Rolls) ya wauguzi na wakunga Tanzania chini ya kifungu 28(3)(a) cha sheria ya uuguzi na ukunga Tanzania ya mwaka 2010 na kutakiwa kurejesha vyeti na leseni  kwa Muuguzi Mkuu  wa Mkoa wa Rukwa ambaye atawasilisha kwa Baraza.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema  haki ya rufaa imeelezwa chini  ya kifungu 31(1) cha sheria ya uuguzi na ukunga Tanzania ambapo anaweza kukata rufaa kwa Waziri Mwenye dhamana ndani ya miezi mitatu tangu tarehe ya hukumu.

Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa  Rais wa Chama Cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Alexander Baluya amewataka wauguzi kufanya kazi kwa weledi licha ya changamoto ya watumishi hasa katika kada ya uuguzi.

Baluya amewataka wauguzi wote nchini  kuishi kwa kufuata miongozo ya taaluma yao kwani kukiuka maadili ya taaluma yao inawaondolea sifa na kuonekana muuguzi sio rafiki wa mteja.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 24, 2021

Mitandao yaipatia Serikali Bil 80 kwa Mwezi
Rais Mwinyi afanya teuzi