Mwanamke aliyekuwa anamshtaki R. Kelly Mahakamani kwa madai ya kumnyanyasa kingono alipokuwa na umri wa miaka 16 ameshinda kesi baada ya mfalme huyo wa RnB kutohudhuria mahakamani bila kutoa taarifa rasmi.

Mlalamikaji huyo alifungua kesi hiyo Februari mwaka huu jijini Chicago na siku kumi baadaye R Kelly alikamatwa na kushikiliwa katika selo za polisi kwa siku kadhaa.

Huyu ni mmoja kati ya wanawake wanne waliokuwa wanamtuhumu R Kelly kwa kuwanyanyasa kingono walipokuwa na umri wa chini ya miaka 18.

Jana, Jumanne wiki hii Jaji wa Mahakama ya Chicago alitoa uamuzi wa kesi hiyo huku upande wa utetezi ukiwa haupo mahakamani.

Jaji Moira Jonson atasikiliza tena kwa mara ya mwisho upande wa mlalamikaji na kutoa uamuzi wa kiasi cha faini ambacho R Kelly anapaswa kulipa.

Mwanamke huyo aliyekuwa analalamika anadai $50,000 sawa na shilingi milioni 115 za Kitanzania kama fidia dhidi ya vitendo alivyofanyiwa.

Kiasi hicho kinaonekana kuwa ni mtihani kwa R.Kelly kwani amethibitisha kuwa amefilisika na kuwa na kiasi cha chini ya milioni tatu za Kitanzania.

Mkoa wa Dar es salaam kinara ukusanyaji mapato
Video: Sugu amuomba kazi Rais Magufuli, aeleza anavyomuunga mkono

Comments

comments