Jeshi la polisi mkoani Dodoma linamshikilia mkazi wa Swaswa jijini Dodoma kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma visu mkewe Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Rose Mndenye kwa kisa kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Katika tukio lililotokea mnamo Mei 25, 2018 maeneo ya Swaswa mtaa wa Sulungai jijini Dodoma ambapo mtuhumiwa huyo alimchoma kisu mkewe na kumsababishia kifo na yeye kutoroka.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Giles Muruto leo Juni 18 amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo akiwa mafichoni kijiji cha Chiwachiwa kilichopo kata ya Mbingu, Ifakara Mkoani Morogoro.

Aidha Muroto amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

 

 

 

Muhimbili yathibitisha kumlaza Mbowe, aanguka ghafla
Kanisa lawabatiza kwa kutumia Pombe

Comments

comments