Mwanaume mmoja raia wa Uingereza aliyekuwa anashikiliwa gerezani kama mahabusu kwa kosa la kumpiga mkewe hadi kufa baada ya kumnyima unyumba, amefariki dunia akiwa gerezani nchini Thailand.

Aljazeera imeripoti kuwa mwili wa mwanaume huyo aliyetambuliwa kama Kevin Smitham ulikutwa kwenye gereza la Ubon Rtchathani Central, na sababu ya kifo chake imetajwa kuwa ni majeraha makubwa aliyokuwa nayo.

Smitham mwenye umri wa miaka 51, alikuwa akisubiria mwenendo wa kesi yake ya kumuua mkewe, Kandra Smitham raia wa Thailand aliyekuwa na umri wa miaka 29, Aprili 15 mwaka jana.

Wawili hao walikuwa na watoto wawili wadogo na walikuwa wanaishi kwa wazazi wa Kandra katika eneo la Ubon Ratchathani, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kwa ajili ya mapumziko ya sherehe za mwaka mpya.

Kevin Smitham na mkewe Kandra

Mwili wa Kandra ulikutwa na majirani ukiwa umefungwa kwenye blanket na kutupwa mbali na nyumba, mapema Aprili 16.

Polisi wanadai kuwa Smitham alimshambulia vibaya mkewe na kumuua, kisha akauficha mwili wake na kurejea kulala kitandani.

Video: Fahamu nyoka hatari wenye sumu kali zaidi duniani
Watu milioni 4.9 wahitaji msaada kwa kukumbwa na njaa

Comments

comments