Komando wa Kikosi maalum chenye hadhi ya pili kwenye Jeshi la Marekani anayeeleza kuwa ndiye aliyempiga risasi Osama Bin Laden na kumuua mwaka 2011 nchini Pakistani, amekamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuvunja sheria.

Rob O’Neill, jana alikamatwa na kikosi cha polisi cha Butte, California akiwa amelala ndani ya gari lake katika eneo la kuegesha magari kwenye eneo hilo na kubainika kuwa alikuwa amelewa.

Afisa wa Jeshi la Polisi la Butte aliiambia CNN kuwa walipokea simu majira ya saa nane usiku kutoka kwa ‘Msamalia Mwema’ na walipofika walimkuta O’Nell akiwa amelala ndani ya gari akiwa hoi. Alisema kuwa Komando huyo alikataa kutoa ushirikiano wa kutumia kipimo cha ulevi.

We woke him up and identified him as Rob O’Neill. He failed a sobriety test and refused a breathalyzer,” alisema George Skuletich, Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi wa Butte, California na kuongeza kuwa walimfikisha polisi na kumfungulia mashtaka ya kuendesha akiwa ametumia kilevi na atafikishwa Mahakamani Jumatatu.

Hata hivyo, baada ya kupewa dhamana, O’Neill aliwaambia waandishi wa habari kuwa hakuwa amekunywa kilevi chochote bali alitumia dawa za kumsaidia kulala kutokana na kuwa na tatizo la kupoteza usingizi. Alisema kuwa anaamini hatakutwa na hatia na watu wote wataelezwa hilo hivi karibuni.

Mwaka 2014, Komando huyo alifanya mahojiano maalum na waandishi wa habari na kueleza kuwa yeye ndiye aliyempiga risasi Osama Bin Laden na kumuua, katika operesheni maalum iliyofanywa na kikosi hicho maalum.

Tanzia: Ndada Kosovo afariki
Kundi la kigaidi la ISIS laibukia Afrika Mashariki