Mmoja wa watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya aliyekuwa miongoni mwa waliomuuzia dawa hizo marehemu rapa Mac Miller hatimaye amehukumiwa kifungo jela baada ya kukiri kosa.

Stephen Walter amekiri kosa la kusambaza dawa za kulevya ambazo zilisababisha kifo cha Miller mnamo 2018.

Kwa mujibu wa sheria za nchini Marekani, Stephen amehukumiwa kifungo cha miaka kumi na saba jela, hata hivyo, mtuhumiwa huyo aliweka wazi kuwa anajuta kwa kuhusika katika kifo cha kijana mdogo ambaye ndio kwanza alikuwa na umri wa miaka 26.

Muuzaji mwingine wa dawa za kulevya Cameron James Pettit alidaiwa kumpa rapper huyo tembe ghushi za oxycodone zilizokuwa na fentanyl na hapo awali alikana hatia.

Inaelezwa kuwa siku mbili kabla ya kifo chake Septemba 7, Mac alipokea dawa mbili za kulevya kutoka kwa Pettit, ambaye inadaiwa alisambaza dawa za oxy za fentany pamoja na cocaine.

Ripoti iliyotolewa na ofisi ya mkuu wa uchunguzi wa mwili wa marehemu Miller ya kaunti ya Los Angeles mnamo mwaka 2019, ilisema rapper huyo alikufa kutokana na “sumu ya dawa iliyochanganywa” haswa fentanyl, coke, pamoja na pombe.

Ripoti hiyo iliainisha kuwa kifo chake kilisababishwa na kuzidisha kipimo cha matumizi ya dawa hizo “overdose’ ya bahati mbaya, mwaka 2018.

Rais Samia azindua barabara ya 85.4 Km, aahidi jambo Tabora
Nyuma ya 'Dakika 23 za CINEMA' ya Maua Sama amesimama FA