Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 33 aliyemwagiwa tindikali na aliyekuwa mpenzi wake amefungua kesi dhidi ya polisi wa jiji la Leicester nchini Uingereza akiwashtaki kwa uzembe.

Kwa mujibu wa mtandao wa Mirror, Daniel Rotariu alimwagiwa tindikali mwaka jana akiwa amelala kitandani, tukio ambalo lilimsababishia upofu wa macho na kumlazimu kuhudhuria kliniki za macho kila wiki.

Ameeleza kuwa ameamua kuwashtaki Polisi kwakuwa amebaini walipata taarifa mapema kuhusu mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Leong kununua tindikali kwa nia ya kumwagia mtu, lakini hawakuchukua hatua yoyote.

Daniel Rotariu

“Walipata taarifa mapema kuwa Katie Leong alikuwa ananunua tindikali mtandaoni lakini walifunika masikio kama hawakusikia na hawakufanya chochote,” Rotariu  amesema.

“Hivi sasa ninaishi katika jela ya kiza kinene. Imeninyang’anya uhuru wangu na uwezo wangu wa kufanya kazi. Imeondolea uwezo wa kuona, sitaweza kumuona mchumba wangu wala mtoto wangu,” ameongeza.

Kitanda alichokuwa amelala Rotariu na eneo lililoharibiwa na tindikali iliyompa upofu

Polisi wa Leicester wameliambia Mirror kuwa wanafahamu kuhusu kuwepo kwa kesi hiyo dhidi yao lakini hawakutoa taarifa zaidi.

Leong na mpenzi wake mpya wa wakati huo, Mark Cummings walishtakiwa kwa kushiriki kumwagia tindikali Rotariu. Lakini jopo la Majaji wa Mahakama ya Leicester lilimuondoa Cummings na kumhukumu Leong kifungo cha maisha jela kwa sharti la kutumikia kifungo chake kwa kipindi kisichopungua miaka 17.

Nicki Minaj adaiwa kufunga ndoa kwa siri
TFF yapata msiba, kiongozi wake aaga dunia