Kijana mwenye umri wa miaka 25, Frank Joseph mkaazi wa jijini Dar es Salaam amekubwa na tukio la aina yake baada ya kuiba mzigo wa mahindi wa kilo 20, hali iliyomlazimu kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Mlandizi mkoani Pwani.

Frank ameeleza kuwa aliiba mzigo huo wa mahindi majira ya saa saba usiku Kibaha mkoani Pwani lakini tangu alipoubeba alishindwa kuutua hadi majira ya saa kumi na mbili asubuhi aliponusuriwa na mmiliki wa mzigo huo.

Katika tukio hilo lililothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Jonathani Shana, baada ya mtuhumiwa huyo kujisalimisha polisi, msako wa mmiliki wa mzigo huo ulichukua saa kadhaa huku mtuhumiwa akiendelea kubeba furushi la mahindi.

“Nilikuwa napita nikaona mzigo upo nje, nikaubeba. Nilivyokuwa naushusha haukutoka kichwani, ulivyogoma kutoka niaamua kurudi kwa mwenyewe lakini sikumkuta hadi nilipokuja kumuona kituo cha polisi,” Mtuhumiwa Frank Joseph alieleza.

Kamanda Mshana alisema kuwa mtuhumiwa huyo alitunzwa katika kituo cha polisi hadi mmiliki alipopatikana na kwamba alipofika alionana na kamanda huyo na zoezi la kumtua mzigo Joseph lilifanikiwa.

Kwa mujibu wa kamanda Mshana, mmiliki wa mzigo huo alimfungua zipu ya suruali mtuhumiwa na kisha akazungumza maneno machache ndipo mtuhumiwa alipofanikiwa kushusha mzigo huo.

Kamanda Mshana amewataka vijana kutojihusisha na wizi na kujikita katika kutafuta mali ya halali ili kuepuka matatizo na mkono wa sheria kwa kuwa raia wema.

 

Akutwa na Sindano tumboni
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 4, 18

Comments

comments