Polisi Mkoani Mara, inamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja kwa kosa la kupanda juu ya nguzo ya umeme, ambapoa kusudio lake bado halijajulikana.

Akithibitisha tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Moses Kaegele amesema mtu huyo alipanda juu ya nguzo ya umeme iliyopo Kijiji cha Mwibagi, kando ya Barbara ya Musoma- Mwanza.

Mtu anayedaiwa kupanda juu ya nguzo za umeem ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mara kwa mahojiano.

Amesema, watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoani Mara walifika katika eneo hilo kisha kumshusha mtu huyo na kumkabidhi kwa polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Uokoaji na Zimamoto Mkoa wa Mara, Agostino Magere amesema, “hadi sasa sina taarifa huyu mtu anaitwa nani, umri wake, makazi yake na lengo la kupanda kule juu hebu tusubiri polisi watabaini nini.”

Waziri wa zamani wa Nishati jela miaka 20 kwa ufisadi
Waandamana kutaka Rais aondolewe madarakani