Uongozi wa Simba SC utamtangaza mchezaji aliyesajiliwa na klabu hiyo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili leo Ijumaa (Januari 14) mishale ya saa Saba Mchana.

Simba SC imetoa taarifa hizo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, huku picha iliyowekwa kwenye taarifa hiyo ikionesha kivuli cha mchezaji atakayetangazwa.

Ujumbe ulioandikwa kwenye kurasa za Instagram na Facebook za klabu ya Simba SC unasomeka: “Saa 7:00 mchana shughuli zote zitasimama kwa muda kupisha utambulisho wa mabingwa wa nchi.”

“Shughuli yote kwenye Simba App #NguvuMoja”

Simba SC imekua kimya tangu Dirisha Dogo la usajili lilipofunguliwa Desemba 16, hali ambayo imekua ikiongeza shauku kwa Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo, kutaka kufahamu nani atatua klabuni kwao.

Sabaya akutwa na kesi ya kujibu
Ahmed Ally: Mbeya City mjipange