Mwanamke aliyekaa kwenye ndoa miaka 24 na kutafuta mtoto kwa miaka 15, Bi Honoratha Nakato kutoka Uganda hatimaye ameandika historia mpya barani Afrika baada ya kujifungua watoto mapacha watano na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza chini ya Jangwa la Sahara kuzaa idadi hiyo kupitia njia ya IVF (kupandikiza mayai).

Kwa mujibu wa Azam tv Mama huyo amekuwa akihangaika kutafuta mtoto kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yeyote mpaka alipopata ushauri wa kutumia mfumo huo wa IVF.

”Nilipofanya uchunguzi na kuambiwa na madaktari kuwa nitajifungua niliona kama ndoto hivi, nilifanya siri kiasi kwamba hata mume wangu hakujua kama nilikuwa natarajia watoto watano, alikuwa anajua angalau wawili,” amesema Honoratha.

Honoratha ameongeza ”Nilihangaika miaka mingi kutafuta mtoto, nilitembea huku na kule hadi nilipokuja kwa dokta Sad, ila wengi walinitisha kuwa nisingeweza kulipia gharama yake na hatimaye nilifikia muafaka ila sikutarajia kupata idadi hii ya watoto.”

Daktari aliyemzalisha mama huyo ameelezea namna alivyo weza kufanya uzalishaji huo huku akishindwa kuamini.

”Ilikuwa muujiza, muujiza kabisa na tofauti na tulivyofanya kabla. Tulifanya upasuaji na mtoto wangu mtoto wa kwanza alitoka kichwa chake kikiwa kimefungunguka nikasema huyu msichana tu wapili hivyo hivyo watatu mvulana,” amesema daktari

”IVF imebadilisha maisha kabisa kiasi kwamba kwa sasa hivi hakuna mwanamke asiyeweza kubeba mimba, mtazamo na hisia za watu zimebadilika kabisa watu hawana aibu tena kwenda kufanya njia hii.”

”Wanne wavulana na watano msichana, sijawahi kumzalisha mwanamke hivi katika miaka yangu 30, yakufanya kazi hii.”

Honoratha amekuwa katika ndoa na amekuwa akishinikizwa na ndugu wa mumewe na jamii kwa ujumla ilimpelekea kutafuta mtoto kwa njia zote hadi kuambiwa kuhusu njia ya upandikizaji mayai licha ya kuwa ni gharama kubwa kifedha huku siku tatu toka kujifungua mume ameshindwa kufika hospitalini kwa mshtuko wa idadi ya watoto.

Shirikisho la Madereva Tanzania (TDF) lapata uongozi mpya
Barabara za juu Tazara zaanza kutumika rasmi leo