Mahakama nchini Marekani imekataa ombi la mwanaume mmoja aliyemtaka mkewe amrudishie figo yake aliyompa mwaka 2001, baada ya mkewe huyo kuomba talaka.

Richard Batista ambaye ni daktari wa upasuaji, alichukua uamuzi huo baada ya mkewe aliyetajwa kwa jina la Dawnell kudai talaka miaka minne tu baada ya kupewa figo. Mwanamke huyo alidai kuwa Batista alikuwa anamfanyia ukatili.

Katika kesi hiyo, Batista alidai kuwa mkewe anapaswa kumrudishia figo yake au kumlipa zaidi ya $1 milioni kama fidia.

Mahakama ya Juu ya Kaunti ya Nassau, katika hukumu yake yenye kurasa 10 ilieleza kuwa haitambui figo kama sehemu ya mali zinazopaswa kubainishwa katika kesi ya madai ya talaka.

Mahakama hiyo ilieleza kuwa kuna mambo mengi ambayo yanaweza kutambulika kama mali za wana-ndoa lakini viungo vya binadamu sio sehemu ya mambo hayo.

Ilieleza zaidi kuwa kitendo cha Batista kujaribu kujipatia fedha kutoka kwa mkewe kupitia figo aliyompatia kisheria kinaweza kumfanya afunguliwe kesi ya jinai.

Siri mgao wa umeme: Waliokausha maji Mtera wafukuzwa na Magufuli
Reli ya SGR kufika Mwanza, Arusha