Geita, usiku wa tarehe 2 Septemba  kijana mwenye umri wa miaka 18, Samson Petro ameshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuteka watoto katika mkoa wa Arusha na Geita.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha taarifa hizo za kukamatwa kwa mtekaji huyo.

Kwa mujibu wa Jeshi la polisi uchunguzi unaendelea na endapo utakamilika atafikishwa mhakamani kwa mahojiano zaidi.

Mwabulambo amesema kuwa kijana huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungului iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto mdogo nmwenye miaka miwili.

Amesema mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha kulala wageni  iitwayo Shitungulu wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Omben Mshana na Elizabeth Ombeni.

Aidha mama mzazi wa mtoto aliyetekwa Elizabeth Omben, amesema anaishukuru Serikali kwa jitihada ilizozionesha za kuhakikisha mtoto wao aliyepotea kwa msaa 36 anaonekana.

Riyad Mahrez aliponzwa na tamaa za kwenda Old Trafford
Real Madrid yaitikisa Inter Milan