Aliyekuwa kinyozi na kutobolewa macho na Scorpion, Said Mrisho yameibuka mazito baada ya kuamua kuikimbia kwa makusudi familia yake ya mke na watoto wanne mmoja akiwa kichanga cha mwezi mmoja.

Stara Soud, ambaye ni mke wa Said amesema hayo yametokea hivi karibuni baada ya wawili hao kuhamia kwenye nyumba ya kupanga maeneo ya Majichumvi.

Said alitumia mbinu ya uongo kuitoroka familia yake na kudai kuwa atasafiri hivyo alimuomba mkewe amtayarishie vitu kwa ajili ya safari yake na kisha akaaga kuelekea kwa rafiki zake, ameeleza mke wake.

Baada ya muda mchache Said alimpigia simu mkewe kumjulia hali kama amekwishamaliza maandalizi ya safari yake, ambapo alivyomaliza kuongea na simu hiyo Said  akasahau kuikata, ndipo mke wake alipofahamu kuwa mume wake Said hakuwa na safari bali alipanga kumtoroka. Sara mke wa said alisikia mazungumzo ya mume wake na rafiki zake wakisema,

” huyu anadhani ninasafiri, nitamkimbia taratibu hadi tuachane kabisa” Said alisikika akisema hayo

Hivyo Sara akaamua kuwajulishe ndugu zake juu ya tukio hilo la kusikitisha lililofanywa na Said na kuamua kumfuatilia Said alipokuwepo na kumkuta akiwa kwenye nyumba yao ya zamani.

Lakini Said hakuonesha ushirikiano kwani alidhamiria alichokuwa anataka kukifanya, hivyo alileta fujo na kuamua kukimbilia mahakani kufungua kesi kuwa mke wake amemwibia shilingi milioni mbili.

Hivi sasa kesi imepelekwa ustawi wa jamii kwa maelezo zaidi.

Rooney awachanganya mashabiki Dar, Mwakyembe atoa neno
Prof. Mbarawa awakalia kooni wamiliki wa Meli na Majahazi