Stanley Irungu raia wa Kenya amefunguliwa shitaka la wizi kwa kosa la kupokea na kutumia pesa zilizotumwa kimakosa kupitia mtandao wa simu wa M- Pesa kutoka kwa mfanyabiashara mmoja aliyejulikana kama Milicent Atieno.

Polisi waliokuwa wanaisimamia kesi hiyo wamesema kuwa wakala wa duka hilo la Mpesa alipewa pesa na mteja ili aweke kwenye namba ya mteja huyo, ila kimakosa alituma pesa hiyo kwa Irungu ambaye pia alikuwa mteja wake.

Ambapo Irungu alitumiwa kiasi cha shilingi 1, 300,000 na katika kiasi hiko aliamua kutoa shilingi 864,000 na kuzitumia huku akijua sio zake.

Hata hivyo mara baada ya kugundua makosa hayo yaliyofanyika wakala alifanya utaratibu wa kuzirudisha pesa hizo ambapo alifanikiwa kurudisha Shilingi 465,000 ambazo zilibaki kwenye akaunti ya simu ya Irungu.

Mbali na kufanikiwa kurudisha kiasi hiko cha pesa jitihada nyingine zilifanyika za kumtafuta Irungu na kumuomba arudishe kiasi hiko cha pesa lakini hazikuzaa matunda, kwani mtuhumiwa huyo hakuwa akipokea simu hiyo.

Mara baada ya kesi kuwasilishwa kituo cha Polisi Irungu alisakwa na kutiwa mbaroni kwa kufanya wizi huo wa makusudi, ambapo alipouliza alikubali kupokea kiasi hiko cha pesa na yupo tayari kurejesha kiasi cha pesa amabcho kimeripotiwa kuibiwa.

”Mheshimiwa nilipokea kiasi hiko cha pesa na kiasi kadhaa nikakitoa, lakini kwa hairi yangu nipo tayari kumrejeshea mlalamikaji pesa yake”. Irungu aliiambia mahakama.

Ambapo baadae aliachiwa kwa dhamana ya shilingi 20,000, na kesi ikafungwa na kusomwa tena Octoba 1 mwaka huu.

Fatma Karume ajibu tuhuma za kusimamishwa Uwakili, 'Mimi bado wakili'
Video: Utaratibu mpya wa ununuzi wa korosho wawekwa hadharani