Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma, linamshikilia Binti mmoja Nasra Khalifa (24), mkazi wa Chamwino ambaye anatuhumiwa kutupa mtoto mchanga aliyejifungua, ambaye alikotwa akiwa amefariki baada ya Wananchi kutoa taarifa juu ya tukio hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, ACP Martin Otieno amesema tukio hilo limetokea hii leo Septemba 14, 2022 katika eneo la Uhindini lililopo katikati ya jiji la Dodoma na kusema mtuhumiwa baada ya kuhojiwa amedai alifanya hivyo baada ya muhusika wa ujauzito kumkataa.

Amesema, ” Mtuhumiwa ambaye tumemkamata sasa hivi anaitwa Nasra Khalifa alienda kupata matibabu kituo cha Afya cha Makole na kudai alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo na kwamba alikuwa akiharisha na kutapika na wakati akipatiwa matibabu aliomba kwenda msalani.”

Matukio tofauti ya utupati wa kichanga katika picha ya pamoja.

Kamanda Otieno amesema, mtuhumiwa huyo alijifungia mlango na alichukua muda mrefu kitu ambacho kiliwapa wauguzi mashaka na walipogongea mlango alikuwa akikaidi kufungua na muda mfupi baadaye akajifungua mtoto wa kiume.

Aidha ameongeza kuwa, baada ya kujifungua mtoto huyo Nasra alikuwa akijitahidi kumtumbukiza kwenye shimo mtoto huyo na hakufanikiwa baada ya kuokolewa na mtoto huyo akawa amefariki Dunia huku mtuhumiwa akidai amefanya hivyo baada ya mtu aliyempa ujauzito kutokuwa na maelewano nae mazuri.

Vitendo vya mauaji ya kikatili, utupaji wa watoto, upungufu wa maadilii na matukio ya kiuhalifu yamekuwa yakiendelea kutokea sehemu mbalimbali nchini, ambapo vyombo vya usalama kwa ushirikiano na Wananchi bado wanaendelea na jitahida za kudhibiti hali hiyo.

Polisi yafafanua tukio la Askari wake kupokea rushwa
Mega Woodcraft wafunguka ujenzi Mo Simba Arena