Mtu mmoja, Shamswadini John (35) mkazi wa Hanang Mkoani Manyara amehukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Manyara, baada ya kupatikana na hatia ya kumua mkewe Asia John (25), na mtoto wake Ahmedi Shamswadini (9) kwa kukusudia.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Devotha Kamzola amesema mshtakiwa Shamswadini alimuua mke wake kwa kumnyonga, na wakati akitekeleleza mauaji hayo mtoto alikuwa akipiga kelele hivyo baada ya kumuua Mama yake akamuua pia na mtoto, na kuchimba shimo kisha kuufukia mwili wa mke wake.

Amesema, wakati akitaka kuufukia mwili wa mtoto alishindwa kufanya hivyo kwa kuhofia kuwa kumeshaanza kukucha na watu watamuona hivyo kuamua kwenda kuutupa mwili wake katika bwawa ili kupoteza ushahidi na uchunguzi wa Daktari, umeonyesha ni kweli walifariki kwa kukosa hewa baada ya kunyongwa.

Awali, Wakili wa Serikali, Petro Ngassa aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine kufuatia mauaji hayo yaliyofanyika Oktoba 31, 2018 katika Kijiji cha Hideti Hanang chanzo cha ugomvi kikiwa ni baada ya mwanaume kuongeza mke wa pili jambo lililomchukiza mke wa kwanza aliyeamua kuhama nyumba.

Baada ya mwanamke huyo kuhama, ndipo Mwanaume aliposhikwa na hasira na kuhisi mkewe ana mahusiano mengine na hivyo kutekeleza mauaji hayo ambapo awali mshtakiwa alikana shitaka na lakini baadae alikiri na kwenda kuonyesha sehemu aliyofukia mwili mkewe na baada ya kufukuliwa ulikutwa ukiwa na kanga shingoni.

Bunge laidhinisha kumuondoa Rais madarakani
Samia, Mwinyi vinara uchaguzi CCM