Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Paul Mubiru, anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uganda baada ya video zake kusambaa katika mitandao ya kijamii akiuza senene ndani ya Ndege ya Shirika la Ndege la Uganda iliyokuwa ikielekea Dubai.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda Fred Enanga, amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa huyo pia Jeshi hilo linamshikilia Hajib Kiggundu, ambaye yeye alihusika katika kurekodi video hiyo.

Kupitia mitandao ya kijamii hivi karibuni zilisambaa video zikionesha Mubiru akiuza Senene, ambapo abiria wengi walionekana kufurahia huduma hiyo kutoka kwake.

Polisi wamesema wawili hao watafikishwa Mahakamani kwa makosa matatu ikiwemo kukaidi maelekezo ya Wahudumu wa Ndege na kuvunja masharti ya Covid 19, wakikutwa na hatia wanaweza kufungwa hadi miaka saba. 

Hata hivyo la Shirika la ndege la Uganda liko kwenye mpango wa kuweka Senene kama sehemu ya chakula kwa wasafiri wa ndani na wa kimataifa

Milioni 460 kwa atakayekubali sura yake itumike kama Robot
RC Makalla apokea vifaa vya kampeni ya usafi