Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Charitable and Development Oganization (TCDO) inayojishughurisha na kusajili, kuhamasisha na kuwasafirisha Waislamu kwenda kufanya ibaada ya Hijja,amenusurika kichapo kutoka kwa waumini wa dini hiyo.

Mwenyekiti huyo anayefahamika kwa jina la Sued Twaibu Sued amekutana na dhahama hiyo katika msikiti wa Nuru uliopo wilayani Muleba Mkoani Kagera alipofika akiwa miongoni mwa taasisi 12 zinazohamasisha Waislamu kujitokeza kwenda kufanya ibaada ya Hijja ambayo hufanyika nchini Saudi Arabia kila mwaka.

Hali hiyo imetokea mara baada ya mmoja wa waumini waliokuwepo msikitini hapo kumuuliza swali kiongozi wa msafara huo aliyejitamburisha kwa jina la Mussa Yusuph Kundecha lililomuhitaji kuwaeleza Waislamu kuwa ni vigezo gani vilitumika kuisajili upya taasisi ya TCDO kwa kuwa mwaka 2017 taasisi hiyo iliwatapeli baadhi ya Waislamu waliojiandikisha kwaajili ya kwenda Makka kufanya ibaada ya Hijja na hadi sasa waumini hao hawajarudishiwa fedha zao.

“Ni kweli nakiri kutokea kwa tatizo hili lililosababishwa na taasisi yangu na kuwafanya Waislamu wengi kutofanya Ibaada hii mnamo mwaka 2017 akiwemo mzee Shaban Khamis, tatizo hili halikutokea kwenye taasisi yangu pekee bali lilitokea kwenye baadhi ya taasisi nyingine lililosababishwa na mtandao kuruka.”amesema Sued

Aidha, ameongeza kuwa hakuwahi kupata nafasi ya kuwaeleza Waislamu juu ya tatizo lililotokea na kuongeza kuwa taasisi yake ina uzoefu mkubwa wa zaidi ya miaka 18 na hakuwahi kukutana na tatizo hilo suala lilosababisha kuwepo kwa kurushiana maneno, ambapo walimtaka kurejesha fedha za waislamu waliotapeliwa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa mmoja wa wale waliotapeliwa na kushindwa kufanya Ibaada ya Hijja ameeleza kuwa aliachwa uwanja wa ndege huku akiwa tayari alikuwa ameshalipia kila alichohitaji kulipia kwaajili ya safari.

  • Video: Lema kifungoni hadi 2020, Uchaguzi serikali za mitaa Oktoba
  • Pierre amuibua Fatma Karume, ‘Kila mtu ana haki ya kuishi atakavyo
  • JPM amfagilia Mkapa, Bila yeye nisingekuwa waziri au Rais

Hata hivyo, kufatia kuwasili kwa taasisi hizo wilayani Muleba, Sheikh wa wilaya hiyo, Sheikh Zakharia pamoja na Imamu mkuu wa wilaya hiyo Ust. Idd Suedi waliwatahadharisha Waislamu kuhusu taasisi zisizo na uaminifu zinazoweza kupelekea kutapeliwa na kushindwa kufanya ibaada takatifu ya Hijja na kuiomba serikali kuzichukulia hatua taasisi zinazowatapeli Waislamu fedha zao ikiwemo kuzifutia usajili.

Video: Wakili Manyama amtaka CAG aachie ngazi, 'Bora ajiuzulu tu'
Rais Magufuli kufanya ziara ya siku 2 mkoani Njombe