Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa alizamia kwenye ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways iliyokuwa inatokea jijini Nairobi nchini Kenya kwenda jijini London nchini Uingereza ameripotiwa kufariki dunia baada ya kuanguka muda mchache kabla ya ndege hiyo kutua uwanja wa ndege Heathrow jijini London.

Mwili wa mtu huyo, ambaye jina lake halijafahamika, ulipatikana katika bustani ya Clapham, ambapo hadi taarifa hizi zilizopokuwa zinatolewa ilikuwa , haijafahamika mara moja chanzo cha kilichosababisha mtu huyo kudondoka kutoka kwenye ndege hiyo.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa tukio hilo ambao unaendelea kufanywa na Polisi, wamesema kuwa mtu huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka jijini Nairobi kwenda London nchini Uingereza.

Aidha, Polisi wamesema kuwa mwili huo utafanyiwa uchunguzi ili kubaini kilichosababisha kifo chake.

Kwa upande wa shirika la ndege la Kenya Airways limesema kuwa ndege hiyo imefanyiwa uchunguzi na hakuna hitilafu yoyote iliyoripotiwa.

“Ndege hii huchukua saa 8 na dakika 50 kukamilisha safari yake. Inasikitisha kuwa mtu aliyepoteza uhai wake baada ya kuingia kwenye ndege yetu kisiri,”amesema Msemaji wa Shirika hilo

Waziri Mwakyembe ateta na mawaziri kutoka Zanzibar, wasaini makubaliano
Simba yazidi kujiimarisha, yashusha kifaa kutoka TP Mazembe

Comments

comments