Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amempongeza Ally Kamwe kwa kitendo cha kutangazwa kuwa Afisa Habari wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans.

Kamwe alitangazwa kuwa mrithi wa Hassan Bumbuli jana Jumanne (Septemba 27) jijini Dar es salaam, baada ya Uongozi wa Young Africans kukamilisha mchakato wa kumpata Afisa Habari mpya.

Ahmed Ally ametoa pongezi hizo kupitia kurasa zake za Mitandao ya kijamii, akimkaribisha Ally Kamwe, huku akisisitiza kutokua na mashaka katika utendaji wake wa kazi.

Ifahamike kuwa wawili hao wamewahi kufanya kazi kwa pamoja wakiwa katika kituo cha Azam Media, hivyo wanafahamina vizuri sana.

Ahmed Ally ameandika: Karibu sana ndugu yangu @alikamwe

Taasisi yako imepata mtu sahihi na naamini utafanya mambo sahihi kwa maslahi ya taasisi na mpira wa Nchi.

Sina mashaka na uwezo wako najua unaweza kufanya makubwa kwenye idara yako.

Karibu ulingoni comrade

Nimefurahi🙏🙏

Kenya: Majina maarufu yakosekana Baraza la Mawaziri
Hujuma yahusishwa shambulio mabomba ya gesi