Baada ya kutangaza kuwa Afisa Habari wa Klabu ya Young Africans, Ally Kamwe amefunguka kwa furaha na kusema hana budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa nafasi hiyo aliyoipata.

Young Africans ilimtangaza Ally Kamwe jana Jumanne (Septemba 27), kushika wadhifa huo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Hassan Bumbuli aliyeondoka klabuni hapo kufuatia mkataba wake kumalizika.

Amesema anatambua ana majukumu mazito ya kuhakikisha anaisemea Young Africans kwa Wanachama na Mashabiki kupitia Vyombo vya Habari, hivyo amewataka wadau wote kumpa ushirikiano, ili kutimiza wajibu wake ipasavyo.

“Ninamajukumu makubwa mbele yangu na matarajio makubwa juu yangu kutoka kwa mashabiki wa Young Africans”

“Kikubwa ninaomba ushirikiano kutoka kwa wadau wote, ili niweze kuifanya kazi yangu kwa urahisi, nina uhakika kila mmoja anayehusika na klabu hii atapata habari kwa wakati kupitia vyanzo mbalimbali.”

Kuhusu kuwa Mwanachama wa Young Africans Ally Kamwe amesema: “Unajua hili suala sio la utani Young Africans waliposema wanataka afisa habari awe mwanachama walimaanisha”

“Mimi ni Mwanachama wa klabu ya Young Africans muda mrefu sana na nimeshiriki shughuli nyingi za klabu kabla. Nimefurahi kupata nafasi hii ya kuitumikia klabu yangu”

“Oktoba 8 tunakwenda kufanya jambo kubwa, Young Africans ni klabu kubwa Barani Africa tunataka kuuonesha ukubwa wetu”

Wakati huo huo Mchambuzi wa Soka kupitia kituo cha Clouds FM Priva Abiud ametangzwa kuwa Mkuu wa kitengo cha Maudhui ya Mtandao wa klabu hiyo.

Naye

CPA Haji Mfikirwa ametangazwa kuwa Mkuu Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki ( Members and Fans Engagement).

CPA Mfikirwa ni msomi mwenye shahada ya biashara na mbobezi wa fani ya uhasibu, alijiunga na Klabu ya Young Africans tangu Mwaka 2020 na amefanikisha maboresho makubwa katika idara ya Fedha na utawala wa Klabu.

Kutokana na utendaji wake mzuri na mafanikio aliyoyapata katika idara ya fedha, uongozi wa juu wa Klabu umefikia maamuzi ya kumhamishia kwenye idara hiyo mpya ambayo ni muhimili Mkubwa katika muundo huo mpya wa uendeshaji wa Klabu.

Miraj Athuman aigomea Geita Gold FC
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 27, 2022