Afisa Habari wa Young Africans Ally Kamwe amewajibu baadhi ya Mashabiki wa Klabu hiyo, waliotoa maoni katika Vyombo vya Habari na kuandika katika Mitandao ya Kijamii, kuhusu matokeo ya mchezo wa jana Jumatano (Novemba 02), dhidi ya Club Africain ya Tunisia.

Young africans iliambulia matokeo ya sare ya bila kufungana katika mchezo huo wa Mkondo wa Kwanza hatua ya mtoano Kombe la Shirikisho Barani Afrika, huku ikitarajia kwenda mjini Tunis-Tunisia kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa Novemba 09.

Baadhi ya Mashabiki wa Klabu hiyo inayoshikilia Taji la Ligi Kuu Tanzania Bara, walionyesha kukasisrishwa na matokeo hayo, huku wakimlaumu Kocha Nasreddin Nabi kwa kushindwa kuwa na mbinu mbadala katika Michezo ya Kimataifa.

Wengine waliutupia lawama Uongozi wa Young Africans kwa kushindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo, hali ambayo wanaamini ilikua sababu ya matokeo ya suluhu, walioyapata.

Ally Kamwe amesema Uongozi wa Young Africans umesikia na kuona maoni yaliyotolewa na baadhi ya Mashabiki hao, na kuahidi watayafanyia kazi kabla ya mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa mjini Tunis-Tunisia.

“Yote yaliosemwa na kuandikwa, tumeyachukua kama Motisha kuelekea mchezo wa Marudiano kule Tunisia” asema Ally Kamwe

Katika mchezo wa Mkondo wa Pili Young Africans italazimika kiusaka ushindi wa aina yoyote ama sare ya mabao ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Nassib Ramadhan atamba kumchakaza Helebe
Mapya yaibuka maambukizi Homa ya Nyani