Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Ally Mayay, amepongeza hatua ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwezesha Kambi ya Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 17 ‘Serengeti Girls’ nchini England.

‘Serengeti Girls’ itashiriki Fainali za Kombe la Dunia chini ya Miaka 17 zitakazofanyika nchini India Oktoba 11–30, huku Tanzania ikipangwa kundi D lenye timu za Mataifa ya Japan, Canada na Ufaransa.

Mayay amesema maamuzi ya Serikali kuipeleka ‘Serengeti Girls’ ni hatua kubwa kimichezo na yataleta tija kwa faida ya timu hiyo na kwa mchezaji mmoja mmoja.

“Ni hatua kubwa sana kwa Serikali kuipeleka England timu hii kwa ajili ya Kambi, watakua huko kwa majuma mawili, nimesikia watacheza michezo ya kirafiki na klabu kadhaa upande wa wanawake,”

“Hii itakua faida kubwa kwa timu kwa sababu itapata uzoefu mkubwa kabla ya kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia, pia itafungua milango kwa mchezaji mmoja mmoja kupata nafasi ya kucheza soka nje ya nchi, kwa sababu ninauhakika Klabu watakazocheza nazo pale England zitavutiwa na uwezo wa wachezaji wetu.” amesema Ally Mayay

Katika Fainali za Kombe la Dunia ‘Serengeti Girls’ itaanza kupapatuana na Japan Oktoba 12, kisha itashuka tena Dimbani Oktoba 15 kucheza dhidi ya Ufaransa, huku ikimaliza dhidi ya Canada Oktoba 18.

AU yataka kiti cha uwakilishi G20
Mtanzania kutumia betri chakavu kuzalisha umeme