Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo nchini Ally Mayay Tembele, ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika Bodi ya Ushauri wa Michezo ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth Advisory Body on Sport – CABOS) na kuwa Mjumbe mwakilishi wa Bara la Afrika.

Uteuzi huo kwa Ally Mayay umekuja baada ya Tanzania kuteuliwa kuwa Mjumbe katika Bodi ya CABOS kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2023-2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) imeeleza kuwa hatua hiyo inatokana na kuimarika kwa nchi ya Tanzania katika nyanja za diplomasia ikiwemo ya michezo katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

CABOS ni chombo cha kumshauri Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Serikali wanachama kuhakikisha kunakuwepo ushirikishwaji thabiti wa Serikali na uwakilishi katika maendeleo ya sera na utekelezaji wake kwa kuzingatia maadili na matarajio yaliyowekwa ndani ya Mkataba wa Jumuiya hiyo.

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), amempongeza Mayay na kumtakia uekelezaji mwema wa majukumu yake.

Kiuzoefu Alli Mayay ni mwanamichezo nguli na Nahodha mstaafu wa Timu ya Taifa ya (Taifa Stars) na ni kocha wa mpira wa miguu kitaaluma.

Changamkieni fusra kujenga uchumi kidijitali: Waziri Mkuu
Kifo cha Mobby chapeleka ujumbe TFF