Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Ally Mayay, amesema hakufahamu chochote kuhusu uteuzi wake, baada ya kutangazwa kupitia Wiziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo juzi Jumanne (Septemba 20).

Ally Mayay ambaye aliwahi kucheza soka katika klabu za CDA ya Dodoma na Young Africans ameteuliwa kushika wadhifa huo, akichukua nafasi ya Yusuph Omary Singo aliyepangiwa majukumu mengine na uteuzi huo umeanza kazi rasmi leo Septemba 20, 2022.

Mayay amesema ilikua kama mshtuko kwake baada ya kupigiwa simu na baadhi ya Waandishi wa Habari wakitaka kufahamu namna alivyopokea uteuzi huo.

Amesema baada ya muda alijiridhisha juu ya taarifa hizo na baadae kuona zikisambaa kwa kasi katika Mitandao ya kijamii, ndipo alipoamini kweli ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini.

“Sikufahamu chochote, nilikua katika eneo langu la kazi nikiedelea na kazi zangu kama kawaida, baadhi ya waandishi wa habari walinipigia simu na kuanza kunipongezana wengine wakitaka kufahamu namna nilivyopokea uteuzi huu.”

“Kwanza sikuamini nilitaka kujiridhisha, lakini wakati nipo kwenye mpango huo kwenye mitandao ya kijamii nako kukawa na taarifa nyingi zikisambaa kwa kasi kuhusu hili, ndipo nilipoamini taarifa hizi zina ukweli.”

“Ni jambo na kumshukuru Mungu kwa sababu hakuna anayeijua kesho yake, imekua bahati kwangu na sina budi kuikubali kwa kuaminiwa na Waziri, hivyo ni jukumu langu kuchapa kazi ili kufanikisha lengo linalokusudiwa.”

“Kuna kazi kubwa ya kufanya, nimepokea magizo ya Waziri Mchengerwa na ninaanza kuyafanyia kazi mara moja ili kwenda sambamba na kazi anayoihitaji katika Michezo.” amesema Ally Mayay

Kabla ya uteuzi wa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mendeleo ya Michezo, Ally Mayay aambaye ameitumikia Taifa Stars wakati wakicheza soka, alikuwa Afisa Mwandamizi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, pia alikua akichambua michezo katika kituo cha Televisheni cha Azam TV.

Kisinda: Nina deni kubwa Young Africans
AU yataka kiti cha uwakilishi G20