Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi amesema almasi ya nchi hiyo si laana na marekebisho yoyote ya muundo wa Umoja wa Mataifa, yatakuwa na maana kwa mataifa madogo kama Botswana ikiwa yatakaporuhusu kila nchi kushiriki kwa usawa katika baadhi ya mambo bila kujali ukubwa.

Katika hotuba yake, aliyoitoa kwenye Mkuu wa mkutano waw a 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA77, Rais Masisi amesema, “mimi na serikali yangu tuna hamu ya kuona wananchi wetu wakiwakilishwa na wakiajiriwa ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa.”

Raia wa Botswana, Collen Vixen Kelapile alichaguliwa kuwa Rais wa Baraza la uchumi na kijamii la mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililomaliza kipindi chake na Rais Masisi anasisitiza kuwa, “Naamini Botswana imeonesha uwezo wake na kupata tathmini nzuri kutokana na usaidizi wao kwa sekretarieti ya ECOSOC wakati wa awamu yetu.”.

Katika hotuba yake, Rais Masisi amegusia pia mchango wa almasi katika uchumi wa Botswana, taifa la kusini mwa Afrika ambalo hivi limevuka kutoka kuwa nchi maskini au nchi ya kipato cha chini na kuwa nchi ya kipato cha kati, na kuwaambia viongozi wanaoshiriki mjadala huo kuwa, wanaweza kuitambua Botswana ya leo ni nchi ya ngazi ya juu ya kipato cha kati.

UN: Hakuna dalili ya kumalizika kwa vita Ukraine
TALIRI yatakiwa kuongeza uzalishaji mazao ya mifugo