Mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain wamejipanga kumsajili mlinda mlango kutoka nchini Italia na klabu ya AC Milan Gianluigi Donnarumma, endapo mlanda mlango wao Alphonse Areola ataondoka katika kipindi hiki cha dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kituo cha televisheni cha Sky Sport Italia, wakala wa mlinda mlango huyo wa AC Milan Mino Raiola atakutana na viongozi wa PSG, kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya awali.

Raiola ambaye pia ni wakala wa Areola, atayatumia mazungumzo na viongozi wa PSG ya kufahamu mustakabali wa mteja wake, ambaye ameonyesha kuhofia hatua ya kusajiliwa kwa mlinda mlango gwiji kutoka nchini Italia Gigi Buffon.

Areola anatajwa kuwa kwenye mipango ya klabu ya AS Roma ya Italia, ambayo imeanza mchakato wa kumsaka mbadala wa Alisson Becker anaeondoka klabuni hapo na kutimkia kwa wababe wa Anfield Liverpool kwa ada ya Euro milioni 75 ambazo ni sawa na Pauni milioni 66.9.

Image result for Alphonse Areola and Gianluigi Donnarumma

Hii ni mara ya pili kwa PSG kuonyesha nia ya kuhitaji huduma ya mlinda mlango Donnarumma, kwa mara ya kwanza walifanya hivyo msimu uliopita, lakini walikabiliwa na vikwazo kutoka kwenye uongozi wa AC Milan.

Endapo Donnarumma mwenye umri wa miaka 19 atafanikiwa kujiunga na PSG, atapata nafasi ya kujifunza kwa ukaribu mbinu za kulinda lango, kutoka kwa gwiji Buffon, ambaye majuma matatu yaliyopita alikamilisha usajili wa kuitumikia klabu hiyo ya jijini Paris.

Steve Nyerere ajibu shambulio la Muna 'nimesamehe'
Picha za utupu zamponza Mobetto, TCRA yafanya maamuzi haya