Kundi la kigaidi la al-Shabab lenye makazi yake nchini Somalia, limekiri kutekeleza shambulizi lililotokea Jumatatu asubuhi nchini Kenya, ambapo askari watano waliuawa.

Shambulizi hilo linaloaminika kutekelezwa na roketi na kulenga gari ya polisi aina ya Land Cruiser lilitokea kilomita chache kutoka mji wa Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.

Mji wa Mandera uko mita chache kutoka mpaka wa Kenya na Somalia.

Radio Andalus iliyoko nchini Somalia imetangaza kuwa, shambulizi hilo ni kuipa Kenya adhabu ya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia. Kenya ina vikosi vyake vya kijeshi nchini Somalia chini ya muungano wa Afrika AMISOM.

Source: BBC

Video: Waziri ameitaka Muhimbili kutoa maelezo baada ya taarifa zilizotolewa na gazeti Mwananchi
Diamond awaweka mashabiki mguu sawa, kulipua Spika punde na ‘P Square’