Uongozi wa Man Utd umeripotiwa kumalizana na Alvaro Morata katika mzungumzo binfasi, ili kukamilisha sehemu ya uhamisho mshambuliaji huyo akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Hispania na barani Ulaya Real Madrid.

Taarifa zilizotolewa na Cadena COPE nchini Hispania zimeeleza kuwa, Man Utd walipewa ruhusa ya kufanya mazungumzo binafsi na mshambuliaji huyo, ili waanze rasmi makubalino na uongozi wa Real Madrid kwa ajili ya ada ya uhamisho.

Jose Mourinho amekua mstari wa mbele kuhakikisha anamnasa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye anaami atafanikisha mpango wa kufanya vyema msimu ujao wa ligi ambao utaanza rasmi Agusti 12.

Mipango ya kusajiliwa na Morata ilipata msukumo mkubwa baada ya Man Utd kushindwa kumpata mshambuliaji wa Ufaransa na klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann, ambaye alisaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Hispania juma lililopita.

Wakala wa Morata, alionekana katika viunga na Bernabeu, saa kadhaa badaa ya viongozi wa Man utd kuripotiwa kukamilisha mazungumzo na mshambuliaji huyo.

Ada ya uhamisho wa Morata ambaye anapewa matumaini makubwa ya kutua Old Trafford inatajwa kufikia Pauni milioni 70.

Kasesela akesha mgodini kuokoa mwili wa mchimbaji
Ibrahim Akilimali: Katiba Inanizuia Nisigombee Uenyekiti