Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini Italia, Juventus Alvaro Morata amewaacha njia panda mashabiki wake, baada ya kujianika katika mitandao ya kijamii akiwa sehemu ya watu waliokua mbele ya bango lililosomeka “Adios Amigo” likimaanisha neno “Kwaherini”.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, alianika picha hiyo katika mtandao wa kijamii wa Instagram, huku kukiwa na fununu zinazomuhusisha na mpango wa kuwa katika rada za usajili wa klabu za Arsenal, Chelsea pamoja na Real Madrid.

Mashabiki kadhaa wamezua maswali mengi vichwani mwao kuhusu bango hilo, lakini mpaka sasa haijaelezwa Morata alikua anamaanisha kama ilivyoeleweka alikua akiwaaga.

Tayari thamani ya usajili wa Morata imeshatangazwa kuwa ni Pauni milioni 51.

Everton Wajipanga Kumnusuru Joe Hart
Leicester City Wamuweka Sokoni Jamie Vardy

Comments

comments