Rais wa serikali ya awamu ya sita ya mapinduzi ya Zanzibar, Amani Abeid Karume ameonesha kuchukizwa na lugha za matusi zilijitokeza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea.

Akizungumza leo katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za urais za CCM, muda mfupi baada ya kada mmoja wa chama hicho kumshambulia kwa lugha za kuudhi mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Duni Haji Duni, rais huyo wa zamani aliwata wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu ili kuendelea kuilinda amani na utulivu wa nchi hiyo.

Kada huyo wa CCM alimtaja Juma Haji Duni kama ‘bwege, jinga na mbumbumbu’, maneno ambayo ni dhahiri kuwa Amani Abeid Karume hakufurahishwa nayo.

“Hata unapoongea na jirani yako aliyemwaga maji machafu mlangoni kwako, hakuna lugha nyingine ya kumweleza zaidi ya matusi?” Alihoji Amani Karume.

Amani Karume aliwasihi wananchi wa Zanzibar kuhakikisha wanatunza amani iliyopo kwa kuwa ahadi tele zinatolewa na wagombea kumi na nne wa urais wa Zanzibar hawataweza kuzitekeleza endapo hakutakuwa na amani.

Rais huyo ambaye alitumia zaidi salamu ya kitaifa ya ‘Mapinduzi’, alihitimisha kwa kueleza kuwa yeye huwa hana tabia ya kumuongelea mtu kwa kuwa uamuzi wa kuteleza hufanywa na mgombea mwenyewe pindi atakapoingia madarakani.

 

JK Awapa CCM Mbinu Mpya Ya Kampeni Ya Ushindi
Muigizaji Wa ‘The Vampire Diaries’ Apata Neema