Mwimbaji wa kike, Amber Lulu ametumia picha ya Diamond iliyozua gumzo kwenye mitandao ya kijamii tangu juzi kama fursa ya kumwaga ombi lake hadharani ili limfikie Bosi huyo wa WCB.

Juzi, Diamond alizua tafrani mitandaoni alipoweka kipande cha video kinachomuonesha akiwa anapiga kazi jukwaani nchini Marekani lakini mguuni amevaa cheni, mtindo ambao ni maarufu kwa wakaazi wa Pwani kama Kikuku, na mara nyingi huvaliwa na warembo.

Hata hivyo, Diamond alikazia zaidi kwa kupost picha nyingine ikimuonesha ametulia baada ya kazi lakini ‘kikuku’ kilionekana kwa ukaribu zaidi mguuni kwake. Huenda Mkali huyo wa Baila alitumia mazingira sahihi kufanya kile ambacho ni kawaida kwa Wamarekani aliokuwa anawapigia show, lakini tafrani nyumbani. Wasanii kama Fabolous na wengine wamekuwa wakivaa Kikuku mara kwa mara wanapokuwa jukwaani.

Amber Lulu alitumia picha hiyo kumuomba Diamond kumpa nafasi ya kuwa Bosi wake na kumuomba ampe mkataba wa kuwa mmoja kati ya wasanii walio chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB). Hakika alijua picha hiyo maarufu itabeba ujumbe wake na kuufikisha mbali.

“Sema mzee wa vikuku, si niwe tu msanii wako jamani kwani unasubiri mpaka uvae kikuku cha pili @diamondplatnumz,” ameandika Amber Lulu.

Amber Lulu ambaye wimbo wake ‘Jini Kisirani’ ulipata mafanikio makubwa zaidi katika muziki wake ukitazamwa zaidi ya mara 2,000 kwenye YouTube, sio msanii pekee mwenye kiu ya kujiunga na lebo ya WCB.

Dar24 imedokezwa na watu wa karibu wa lebo hiyo kuwa msululu wa wasanii kadhaa wanaoomba kuingia kwenye lebo hiyo huwa wanapanga foleni kufanya mazungumzo ya kuwasilisha maombi yao, lakini wengi juhudi zao hugonga mwamba.

Walio ndani ya WCB ni pamoja na Rich Mavoco, Lavalava, Harmonize, Ray Vanny, Mbosso na wengine.

Video: Rais Magufuli afungua Mkutano wa Dunia wa Vyama vya Siasa
Video: Nape aitega Serikali, CCM yaandika historia mpya

Comments

comments