Amber Rutty aliyejisalimisha polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi kinyume cha maumbile na kusambaza video ya tukio hilo, leo amefikishwa Mahakamani jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka dhidi yake.

Kamera za waandishi wa habari zilimmulika Amber Rutty alipokaa ndani ya Mahakama, kabla hakimu hajaingia, ambapo alilalamika kuwa anaumwa baada ya afisa wa mahakama kumtaka akae wima kwani hairuhusiwi kuinama ndani ya mahakama.

“Naumwa, nashindwa kukaa. Jana nilipelekwa hospitalini [kupimwa]. Nilipelekwa theater,” alisema Amber Rutty, kauli ambayo ilisababisha afisa huyo wa kike kumruhusu.

“Pole shoga yangu, mwacheni basi akae hivyo anaumwa. Haya [waandishi wa habari] mwacheni ni mgonjwa, asanteni jamani,” alisema Afisa huyo.

Msichana huyo anatuhumiwa kuvunja sheria kwa kushiriki kufanya mapenzi kinyume cha maumbile pamoja na kusambaza video za uchafu huo.

Alijisalimisha Polisi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kumtaka afanye hivyo ndani ya saa 12.

Video: Foby aeleza alivyomlilia mpenzi studio, ‘Niokoe’
Kadinali aliyemkosoa Rais ajiuzulu

Comments

comments