Meneja wa Kiungo Mshambuliaji wa Dodoma Jiji FC Dickson Ambundo amefichua ukweli wa mchezaji huyo kuwa karibu kujiunga na Young Africans, iliyodhamiria kukiboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kimataifa.

Ally Abdallah, meneja wa kiungo huyo mwenye uwezo wa ajabu, amesema suala la mchezaji wake kujiunga na Young Africans lipo katika harakati za kukamilishwa, na kwa sasa amekwenda jijini Dododma kufanikisha sehemu ya dili hilo.

“Kweli nipo Dodoma na hapa namwangalia kijana akiwa mazoezini, kiufupi dili lipoa katika hatua nzuri na kilichobaki ni mchezaji kusaini tu, kuna baadhi ya vipengele vinawekwa sawa ila atasaini Young Africans.”

Hata hivyo, tetesi zinadai kuwa mchezaji huyo tayari ameshawekewa pesa zake za usajili Milioni 50 kwenye akaunti, ili kuepusha janja ya klabu nyingine za Tanzania katika kukamilisha usajili.

Eriksen kupandikizwa betri kifuani
RC Mwanza ampa Mkaguzi Mkuu siku 7