Habari Njema, Rapper Ambwene Yessayah maarufu kama AY Alhamisi hii ameamua kumvisha pete mchumba wake wa muda mrefu Remy, raia wa Rwanda ambaye amekuwa naye kwenye mahusiano tangia mwaka 2008.

Kwa mara ya kwanza Remy alitambulishwa rasmi na Rapper AY siku ya tarehe yake ya kuzaliwa disemba mwaka jana, leo hii tarehe 14 julai 2017, amevalishwa pete ikiashiria ndoa kufungwa hivi karibuni.

MwanaFa, msanii lakini pia rafiki wa karibu wa AY, ametumia ukurasa wake wa instagram kumpongeza AY kwa maamuzi na hatua kubwa ya kimaisha aliyoichukua ambayo vijana wengi hususani wasanii wanaiogopa.

 

Juventus Yaendelea Kujiimarisha, Yamuita Costa
Shughuli za mahakama zakwama nchini Uganda