Nchini Kenya kumetokea kisa kimoja cha kustaajabisha ambapo Wanaume wawili walikubaliana kubadilishana wake baada ya mmoja wao kumfumania mwenziye na mkewe katika ”Mazingira” tatanishi.

Hata hivyo makubaliano yao yalitibuka majuzi baada ya mume aliyenaswa akichovya asali ya mwenziwe kutishia kutengua mkataba huo kwa sababu ya upweke.

Yamkini Bw. Patrick Mangala, 25 ambaye ni mhudumu wa pikipiki za uchukuzi zinazofahamika   kama ‘bodaboda’ alimtishia maisha mume wa ‘mkewe’ kuwa angemtoa uhai iwapo hatamrejeshea mkewe.

Aidha Bw. Ernest Anjeche, 42 ambaye tayari alikuwa kesha onja asali ya mke wake ”mbichi” na mchanga zaidi kwa umri ,amekataa kata kata kurejesha ”kibuyu”.

Anjeche amegundua ubora wa kijana jike huyo Susan.

”Mimi na mwenzangu Mangala tulikubaliana kuwa kwa sababu alikuwa akiiba mke wangu nikiwa nimekwenda kazini heri basi amchukue kabisa waishi naye.

Hata hivyo sifahamu tena kilichotokea kwa sababu yeye ndiye aliyerudi kwangu akimdai Susan eti kuwa mwenzake amemkimbia” Alisema bawabu wa usiku bw Anjeche.

Patrick Mangala, 25 ambaye ni mhudumu wa pikipiki za uchukuzi Bodaboda

Anjeche aligundua mkewe alikuwa amesaliti penzi lake na uchunguzi wake ukabaini kuwa mkewe alikuwa akiondoka kila usiku kushiriki ”wizi” wa mapenzi na kijana huyo.

Mke ‘mpya’ wa bawabu huyo Susan naye ameganda kama gundi hataki kurudi alikotoka.

“Bwanangu alikuwa anatoka asubuhi akienda kazi atarudi keshoye asubuhi. Nikimuuliza unatoka wapi ananiambia eti natoka kazi,” Susan aliiambia runinga ya NTV.

Tatizo lilitokea baada ya majuma mawili  baada ya mpenzi wa siri wa mwendesha boda boda huyo mwenye umri wa miaka 25 alipomtoroka.

Mangala sasa anamtaka mkewe wa zamani Susan arejee nyumbani.

Anjeche, tayari ameripoti kisa hicho kwa polisi akidai kutishiwa maisha na kuwa Mangala alikuwa ”amekiuka mkataba”

“Lakini huyu amekataa, Amesema hawezi toka hapa, atakaa tu hapa na mimi nikasema sawa sawa huyo mke aliyenitoroka akija na akubali kukaa hapa kama mke wa pili pia yeye anakaribishwa” alisema Anjeche.

Rangers Wakamilisha Usajili Wa Niko Kranjcar
Korea Kaskazini Yaichokoza Marekani