Mashabiki wa soka Amerika kusini wametajwa kuwa na kasi ya ajabu ya kununua tiketi za michezo ya fainali za kombe la dunia zitakazoanza Juni 14 nchini Urusi, tofauti na ilivyo katika mataifa ya bara la Ulaya.

Shirikisho la soka duniani FIFA limetoa taarifa za maendeleo ya mauzo ya tiketi ya fainali hizo, na kueleza namna mashabiki wa Amerika kusini wanavyo zichangamkia kwa kasi kubwa.

Kwa mujibu wa FIFA, mpaka sasa tikezi 394,433 zimeshauzwa miongoni mwa tiketi 216,134, na imeonyesha kasi imekua hafifu sana kwa mataifa ya Ulaya likiwepo taifa mwenyeji wa fainali hizo (Urusi).

Mashabiki kutoka nchini Marekani wameshanunua tiketi 16,642 na kuwa miongoni mwa mashabiki wengi wanaotoka katika taifa moja kuchangamkia manunuzi ya tiketi hizo.

Taifa linalofuata kwa manunuzi makubwa ya tiketi hizo ni Argentina (15,006), Colombia (14,755), Mexico (14,372), Brazil (9,962) pamoja na Peru (9,766).

Taifa la Ujerumani ambalo ndio mtetezi wa kombe la dunia limekua taifa pekee la ulaya linalooongoza kwa manunuzi ya tiketi mpaka sasa, kwa mashabiki wake kununua tiketi 5,974, huku China ikifuatia (6,598), Australia (5,905) na India (4,509).

China na India ni miongoni mwa mataifa ambayo hayatoshiriki fainali za kombe la dunia za 2018.

Hata hivyo FIFA hawajatoa taarifa za kina kuhusu manunuzi ya tiketi nyingine 1,698,049 ambazo zinatarajiwa kuuzwa katika mataifa mengine duniani kote, hadi kufikia April 18.

Teknolojia ya kuwakumbusha wagonjwa wa ukimwi kufuatilia matibabu yavumbuliwa
Miguna abanwa na sheria, atakiwa kuomba uraia upya