Bondia kutoka nchini England, Amir khan anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na bondia kutoka Mexico, Saul Alvarez kuwania mkanda wa WBC katika uzito wa kati mnamo Mei saba mjini Las Vegas, Marekani.

Khan mwenye miaka 29, ambaye ni bingwa wa dunia katika uzito wa welter hajapigana tangu apigwe na Chris Algieri mjini New York mwezi Mei mwaka 2015.

Kwa upande wake Alvarez mwenye miaka 25, amewahi kumpiga bondia Miguel Cotto kwa pointi mjini Las Vegas Mwezi Novemba mwaka 2015.

Mpaka sasa Alvarez amepoteza pambano mara moja huku akishinda mara 46 katika mapambano yake.

Mengine Yaibuliwa Kuhusu Uhamisho Wa Neymar
Hiddink: John Terry Bado Ana Nafasi Ya Kuchagua