Mtoto wa miezi miwili mkazi wa Manispaa ya Shinyanga  amenusurika kifo baada ya kunyeshwa sumu na baba yake mzazi, Edson Damian (37) kwa madai ya kutaka kumficha mkewe asijue amezaa nje ya ndoa.

Tukio hilo limeelezwa na mama mzazi wa mtoto huyo, Maria Shija (22) ambaye ameweka wazi kuwa tukio hilo lilitokea Machi 24, mwaka huu, ambapo baba wa mtoto huyo alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo akidai kumsalimia mtoto wake ndipo alipomnywesha sumu ya panya kwa lengo la kumuua.

Amesema kabla ya kumnywesha sumu mtoto huyo, mwanaume huyo alimtuma maji ya kunywa zaidi ya mara ya moja jambo ambalo halikuwa la kawaida amesema Maria.

Maria ameeleza kuwa aliporudisha kikombe ndani ndipo aliposikia harufu ya dawa ya panya na aliporudi alikuta mtoto wake ameanza kutoa mapovu na mwanaume akiwa amekimbia na kopo la sumu ya panya.

”Nilipobaini kuwa mtoto kapewa sumu nikakimbia kwa jirani anayefuga ng’ombe, ndipo nikachukua maziwa nikamnywesha na baadaye nikachukua bodaboda hadi kituo cha polisi kupewa RB na kisha kwenda hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kupatiwa matibabu na sasa mtoto wangu ni mzima,” amehadithia Maria.

Maria amemtaja mwanaume huyo kuwa ni Katibu wa CCM Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Aidha, Maria amesema kuwa wakati mwanaume huyo anamtongoza alimdanganya kuwa hana mke ila mara baada ya kuzaa nae mtoto aliyejaribu kumuua ndipo aliposema kuwa ana mke na hamtaki tena kwani atavunja ndoa yake.

 

NHIF: Tumejipanga kuandikisha watoto 1,000 kwa siku
Arsenal yatinga nusu fainali Europa