Mwenyekiti wa kijiji cha Samanga Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Wilfredy Minja anadaiwa kumshambulia na bakora Asha Rajabu (28) ambae ni mjamzito na kumsababishia maumivu makali.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo, amesema binti huyo alishambuliwa kwa bakora na mtuhumiwa huyo sehemu za makalio na mapajani na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Kamanda Makona amesema kuwa Jitihada za kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa zinafanyika na chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa, tayari timu yangu kwenda Marangu ili kujua ni kweli alikuwa na silaha hiyo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Moshi, Rajabu Kundya amekiri kupokea taarifa za tukio hilo na kwamba, amelielekeza jeshi la polisi kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo ujauzito wa Asha Rajabu, uliharibika kutokana na kipigo cha mwenyekiti huyo ambae pia inadaiwa alikuwa na bastola na kuifyatua juu, Asha yupo katika hospitali ya Kilema Wilayani Moshi akiendelea na matibabu.

Ibenge: Simba SC imejiandaa vizuri
Mwakalebela aikosoa Simba Super CUP